Mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imewanoa wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuhusu usimamizi na udhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara ili wazaidie kupunguza na kutokomeza kabisa ajali baada ya kuwapatia semina maalumu.
Semina
hiyo maalumu ya siku mbili iliyoanza juzi mjini Morogoro
imewashirikisha viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (
TABOA) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Taifa, Mohamed Hood, na kufunguliwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka.
Dk
Mwinjaka katika hotuba yake ya ufunguzi, aliwataka wamiliki wa mabasi
kuwatumia madereva wenye weledi ili kupunguza ajali ikiwa na hatua
ya kuwaendeleza kielimu katika vyuo vya serikali na vya ufundi stadi
Veta.
Mbali
na hayo, aliwataka wamiliki wa mabasi kushirikiana na vyombo vingine
kwa ajili ya kubaini mienendo ya madereva wao hasa suala la ulevi
wanapokuwa kazini na mwendokasi, wakitambua mabasi yao wameyanunua kwa
gharama kubwa na pia yamebeba uhai wa maisha ya binadamu.
Hata
hivyo, alisema aliwahakikishia wamiliki wa mabasi ya masafa marefu
kuwa, Kamati iliyopewa jukumu ya kuangalia namna ya kurekebisha sheria
za makosa yanayowahusu wamiliki na kwa madereva wao imefikia hatua nzuri
na muda si mrefu utawekwa hadharani.
Pamoja
na hayo, pia aliwataka wamiliki wa mabasi kuhakikisha wanakuwa karibu
kufuatilia kila jambo linalofanywa na dereva wake, kwani mwisho wa yote
basi litabaki kuwa ni mali ya mmiliki na dereva ni mfanyakazi wake.
Naye
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga
alisema ajali za barabarani zinazohusisha mabasi hazitaweza kupungua
iwapo sheria na kanuni za mwaka 2007 kanuni 317 hazitazingatiwa na
wamiliki wa vyombo hivyo sambamba na madreva wao.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment