Serikali imesema Tume ya Utumishi wa Walimu itaanza kazi Julai mwaka huu na kuhudumia walimu katika masuala mbalimbali huku muundo wa utumishi wa tume hiyo umehusisha ngazi za chini na juu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani
alisema serikali imekubali kuanzisha tume hiyo ya kuhudumia walimu
nchini ili kuepuka walimu kuhudumiwa na wizara mbalimbali.
Alisema
tume hiyo itaanza rasmi mwezi huo na kuingizwa kwenye bajeti ijayo,
huku madeni ya walimu ya mishahara yakiwa ni yaliyohakikiwa Sh bilioni
sita na ambayo hayajahakikiwa ni Sh bilioni tatu.
Alisema
ili kukabiliana na madeni ya walimu, sasa serikali imeagiza taasisi
zote ziweke kipaumbele katika malipo ya likizo iwe kulipwa mapema kama
mishahara.
Awali,
Kamati ya Huduma za Jamii ilitaka walimu nchini kusajiliwa ikiwa ni
pamoja na wanaofanya kazi katika shule binafsi ili kuwatambua walimu na
kuweka kiwango cha msingi cha kutoa huduma kwa walimu nchini kwa
kuitumia Tume ya Utumishi wa Walimu.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Margaret Sitta alisema kamati inapongeza kusudio la
serikali kuanzisha Tume ya Utumishi wa Walimu nchini katika mwaka wa
fedha 2015/16.
Alisema
kamati inashauri tume hiyo kuanzishwa haraka ili kukabiliana na adha
zinazowakabili walimu nchini na kurejesha hadhi ya taaluma ya ualimu
nchini.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment