Mrembo
na mwigizaji wa Bongo Movies ,Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amedaiwa
kumuumbua shosti wake wa zamani, Kajala Masanja kwa kumwaga ‘ubuyu’
kwamba amefilisika baada ya kigogo maarufu kama CK anayedaiwa kuwa ndiye
mpenzi wake, kuyumba kiuchumi.
Kigogo huyo aliyewahi kuwa na uhusiano na Wema kisha kumwagana naye,
imedaiwa kuwa ile jeuri ya kununua magari ya kifahari, kumiliki biashara
mbalimbali mjini, kwa sasa ameangukia pua kwani hawezi tena
kujitutumua.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na Wema, baada ya
kuhamishia majeshi kwa Kajala, Wema hakufurahia hivyo aliposikia uchumi
umeyumba, amefurahia sana kufuatia ule msemo wa ‘adui muombee njaa.’
“Wema amefurahi sana, anawaambia marafiki zake kuwa malipo ni
hapahapa duniani, Wema alimlipia Kajala dhamana ya sh mil. 13 ili
asifungwe kwa msala wa kutakatisha fedha uliokuwa ukimkabili lakini
akamgeuka na kumchukulia bwana wake, ule si ubinadamu kabisa,” kilisema
chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, Kajala ana nuksi kwani CK alipokuwa na Wema alikuwa na mafanikio na kupata fedha kila kukicha lakini alipohamia kwa Kajala mambo ndiyo yakaharibika.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, Kajala ana nuksi kwani CK alipokuwa na Wema alikuwa na mafanikio na kupata fedha kila kukicha lakini alipohamia kwa Kajala mambo ndiyo yakaharibika.
“Kajala ana nuksi, CK alipokuwa na Wema walikuwa wanapata fedha nyingi kila wakati lakini kwa Kajala wamefilisika kwelikweli,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Madam mwenyewe amemshangaa sana CK kuishiwa fedha wakati alikuwa mtu
wa kucheza na dola nyingi kila kukicha na aliwekeza fedha zake katika
miradi mbalimbali.”
Jitihada za kumpata CK ili azungumzie ishu ya kuyumba kiuchumi
hazikuzaa matunda lakini kwa mujibu wa mmoja wa watu ambao wanafanya
naye kazi, kigogo huyo ameporomoka kiuchumi kwa kile kilichodaiwa kuwa
ni kufanya magumashi ya fedha kazini hadi kufikia hatua ya kutaka
kufukuzwa kazi.
“CK hayuko vizuri kazini, ana majanga kibao, ile jeuri aliyokuwa
akifanya na Wema na Kajala ilikuwa ni fedha za magumashi sasa kimemnukia
kazini,” kilisema chanzo hicho ingawa mwenyewe alipotafutwa kwenye simu
hakupatikana.
Wakati mwanahabari wa Ally Tz Blog akiendelea kuichimba habari hiyo, alifanikiwa kunasa ‘clip’ ya sauti ya Wema iliyoonesha dhahiri kwamba mrembo huyo amefurahishwa na kitendo cha wawili hao kukalia kuti kavu.
Sauti hiyo ya Wema inasikika akizungumza na shosti yake kumueleza
jinsi gani Kajala ameumbuka maana alifikiri kutembea na shemeji yake
ameula kumbe matokeo yake ameangukia pua kwani mwanaume
amefilisika.“…Kajala sasa hivi anaendesha Noah (Toyota) ile yenye
mastikamastika nakwambia…” ilisikika sehemu ya clip hiyo.
Paparazi huyo alimvutia waya Wema ili aweze
kufunguka zaidi kuhusiana na sakata hilo namna ambavyo amefurahia, simu
yake iliita bila kupokelewa.Hata hivyo, mwandishi wetu alikwenda
nyumbani kwake, mtaa wa Bwawani-Kijitonyama jijini Dar zaidi ya mara
tatu kwa nyakati tofauti lakini hakufanikiwa kumpata baada ya mlinzi
kudai amelala.
Mwanahabari alimvutia waya Kajala ili kusikia naye anasemaje
baada ya kudaiwa kuanguka kiuchumi, simu yake iliita bila kupokelewa
lakini hata hivyo, rafiki yake wa karibu ambaye hakutaka jina lake
liandikwe gazetini alikanusha madai ya kufilisika.“Kajala hajafilisika
na hawezi kufilisika, hayo yatakuwa maneno ya watu tu,” alisema rafiki
huyo wa Kajala.
Wema na Kajala waliwahi kuwa mashosti wa damu kabla ya kugombana
ambapo chanzo kilitajwa kuwa ni CK, mwaka jana walidaiwa kupatana
lakini baadaye ikaelezwa kuwa bado wanaendeleza bifu.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment